KUTOKANA na Watanzania takribani 1,000 kukamatwa kwenye nchi mbalimbali duniani, wengi wao wakiwa China kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya ndio sababu inayosababisha kupekuliwa zaidi wanapofika nchi za nje.
Kwa mujibu wa taarifa ya hali ya dawa hizo kwa mwaka 2017 iliyotolewa mwishoni mwa wiki bungeni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye ulemavu, Jenista Mhagama, alisema dawa hizo zimekuwa na madhara mbalimbali ikiwamo ya kidiplomasia.
Alisema kuwa hatua hiyo imechafua taswira ya nchi katika medani ya kimataifa.
"Watanzania wanapofika katika nchi za nje wamekuwa wakipata usumbufu mkubwa wa kupekuliwa zaidi kwa kudhaniwa kuwa wanaweza kuwa wamebeba dawa za kulevya," alisema taarifa hiyo.
Kuhusu takwimu za watumiaji, alibainisha kuwa kutokana na makadirio yaliyofanyika mwaka 2014 Tanzania ilikadiriwa kuwa na watumiaji wa dawa hizo aina ya heroin kati ya 250,000 hadi 420,500 na kati yao 30,000 wakitumia dawa hiyo kwa kujidunga.
Pia alisema wengi wa watumiaji wa heroin wanapatikana kwenye miji mikubwa hasa Dar es Salaam, Tanga, Mwanza, Mbeya, Pwani, Morogoro, Dodoma na Arusha.
Mhagama alisema pamoja na kutunga sheria na jitihada zingine nchi inaendelea kukabiliana na biashara na matumizi ya dawa hizo.
Aidha, alisema kutokana na kutambua ukubwa wa athari zinazosababishwa na tatizo hilo serikali kwa kushirikiana na wadau wa ndani na nje ya nchi imefanya jitihada mbalimbali za kukabiliana nalo.
"Jitihada hizi ni pamoja na kuimarisha ukusanyaji wa taarifa mbalimbali za kiintelijensia, ukamataji wa wauzaji na wasambazaji wakubwa na kuwachukulia hatua wasiofuata taratibu za uingizaji, utunzaji, usambazaji na utumiaji wa kemikali bashirifu," alisema.
Alisema kutokana na kuimarisha udhibiti wa dawa hizo mipakani, kumekuwa na ongezeko la dawa za heroin zilizokamatwa kutoka kilo 42.26 kwa mwaka 2016 hadi kufikia kilo 185.557 kwa mwaka 2017.