Hamisa Mobetto amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuzichukua akili za mashabiki wake mara baada ya hivi karibuni kuanza kuonekana na mwanaume ajulikanaye kama Josh nchini Marekani. Wengine waliamini na Hamisa aliwaaminisha kuwa huyo ni mpenzi wake lakini inavyonekana sivyo.
Josh ametokea kwenye video ya wimbo wa Hamisa akiwa kama King video hivyo bila shaka zile stori za kuwa wapenzi zitafifia pole pole.
Kwanini Alikiba
Kabla ya Alikiba kutoka wimbo wake uitwa Seduce Me, August 25, 2017 aliweza kuwashika mashabiki wake vilivyo pindi walipokuwa wakisubiria ujio wake baada ya kukaa kimya kwa zaidi ya mwaka mmoja bila kutoa wimbo wowote.
Moja ya vitu vilivyowachanganya wengi ni kutaka kujua jina la ngoma mpya ya Alikiba. Wengi waliamini ngoma mpya ingeitwa Kipusa pindi alipoweka cover yenye jina hilo katika ukurasa wake wa Instagram.
Achilia mbali Kipusa, aliweza kuweka cover zenye maneno kama Heart Breaker na Pasua Kichwa kitu ambacho kilifanya baadhi kuamini tena anaweza kutoa ngoma tatu kwa wakati mmoja, kumbe changa la macho.
Watangazaji wa kipindi cha Shilawadu kinachoruka Clouds TV, walifunga safari hadi nyumbani kwa Alikiba. Lengo la safari yao ni kumsaka huyo Kipusa, kujua mengi kuhusu Kipusa.
Katika mazungumzo yao ndani ya dakika moja neno Kipusa lilijitokeza zaidi ya mara tatu. Hivyo na wao waliamini ngoma mpya ya Alikiba inaitwa Kipusa, kumbe sivyo.
Baada ya muda ngoma mpya (Seduce Me) hii hapa, Kipusa Heart Breaker na Kichwa ni maneno tu ya kawaida ambayo yapo katika ngoma hiyo ingawa yamejirudia mara kwa mara.Ndicho alichofanya Hamisa Mobetto kwenye wimbo wake huu mpya, Tunaendana, baada ya mashabiki kukolewa na stori za kuwa mrembo huyo amezamia kwenye penzi jipya nchini Marekani, ameamua kuzitoa fikra zao huko na kuwaleta kwenye muziki.
Hamisa sio wa hivyo
Wanaofuatilia maisha ya kimahusiano na Hamisa Motto wanajua ni kwa kiasi gani mrembo huyo alivyomsiri kwenye mapenzi. Akiwa kwenye mahusiano mtu ni vigumu sana kuyakweka wazi.
Mrembo huyu ambaye ni mama wa watoto wawili ambao amezaa na watu maarufu Bongo, Majey na Diamond, ni vigumu kupata picha akiwa na wazazi wenzake. Hii ina maana anapokuwa kwenye mahusiano si utamaduni wake kuonyesha mbele ya watu.
September 21, 2018 kwenye mahoajino na kipindi cha The Playlist cha Times FM alisema anapokuwa kwenye mahusiano na mtu siku zote amekuwa akifanya siri hata ikitokea watu wakajua ni kupindi ambacho mapenzi yao yanakuwa yameisha kabisa.
