Na. Thabit Madai,Zanzibar.
Mkutano wa kumi na kumi na mbili wa Baraza la wawakilishi Zanzibar unatarajiwa kuanza siku ya Jumatano Tarehe 28 November saa 3 asubuhi katika ukumbi huo uliopo chukwani nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ofisini kwake chukwai mjini magharib Unguja katibu wa Baraza la wawakilishi Zanzibar Raya Issa Msellem alisema kikao hicho cha kumi na mbili cha baraza la wawakilishi kinatarajiwa kuanza na shughuli za maswali na Majibu pamoja na kuwasilishwa miswada ya sheria.
Alisema jumla ya maswali 123 yameratibiwa kwa ajili ya kujibiwa katika mkutano huo pamoja na kuwasilishwa na kusomwa kwa kwa mara ya pili miswada mitatu ya sheria ambayo iliwasilishwa katika kikao cha mwezi septembar.
Pia alisema mswada utakao jadiliwa ni mswada wa sheria ya kuweka masharti yanayosimamiwa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria, kurahisisha upatikanaji wa haki na kuweka masharti mengine yanayohusiano na hayo.
Mswada mwigine utakaowasilishwa na kujadiliwani mswada wa sheria ya kufuta sheria ya ukuzaji na kulinda vitega uchumi zanzibar namb 11 ya mwaka 2004 na kutunga sheria ya Mamlaka ya ukuzaji na kulinda vitega uchumi zanzibar na kuweka masharti mengine yanayohusiana na hayo.
Pamoja na mswada wa sheria ya kufuta sheria ya vyama vya ushirika namb4. Ya mwaka 1986 na kutunga sheria ya vyama vya ushirika zanzibar ya mwaka 2018 ambayo inaweka utaratibu wa uundwaji na uendeshaji wa vyama vya ushirika na mambo mengine yanayohusina na hayo.
Aidha alisema katika kikao hicho cha kumi na mbili cha baraza la wawakilishi kutatolewa Taarifa ya Serikali kuhusu hoja ya Mjumbe ya kutoa Azimio la kuitaka Serikali kuja na Mikakati unaotekeleza kwa kutatua changamoto zinazowakabili wakulima wa zao la mwani.
Hata hivyo kutawasilishwa hoja ya Mjumbe kuhusu wajumbe wa Baraa la wawakilishi kutoka viti Maalum vya wanawake kufaidikiana fedha za mfuko wa maendeleo wa Jimbo.
“hoja nyingine itakayo tolewa na serikali hoja ya mjumbe wa baraza kuhusu tathimini na ufuatiliaji wa miradi zanzibar” alisema katibu wa Baraza Raya Issa Msellem.
Mkutano huo wa kumi na mbili wa baraza la wawakilishi na unatarajiwa kumaliziaa tarehe sita mwezi wa kumi na mbili mwaka huu.
