Mashabiki wataka Amunike afutwe kazi


Kama utani vile lakini ndiyo hali ilivyo kwa mashabiki wengi wa soka hapa nchini wamelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumfukuza kazi mara moja Kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike.

Hatua hiyo imekuja na kikosi cha timu hiyo kuambulia kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Lesotho katika harakati za kuwania kufuzu kuelekea AFCON huko Cameroon mwakani.

Mashabiki wengi wameeleza kutoridhishwa na upangwaji wa kikosi cha Stars na Amunike jambo ambalo wanaamini limesababisha kupoteza kizembe.

Wengi wao wamesema kitendo cha kuwaacha nje wachezaji kama Feisal Salum, Jonas Mkude na John Bocco kumesababisha timu ishindwe kuonesha kiwango chake.

Wameeleza timu ilikuwa na mapungufu zaidi haswa sehemu ya kiungo wakiamini kukosekana kwa Mkude imekuwa kama pigo ambapo kikosi kiliwa hakina mhilimili mzuri katika safu hiyo.

Stars sasa inapaswa kuiombea Cape Verde iweze kuifunga Lesotho au kwenda sare mechi ijayo huku nayo ikitakiwa kuwafunga Uganda, The Cranes ili kupata nafasi ya kushiriki Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCONN) mwakani nchini Cameroon.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items