Rayvanny awakaushia BASATA kuufuta wimbo wa Mwanza




Baada ya Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kumtaka Msanii wa Muziki Rayvanny afute wimbo wake mpya wa Mwanza aliomshiirikisha Diamond Platnumz kwenye mitandao ya kijamii kabla ya saa 10:00 jioni ya leo Novemba 12,  Msanii huyo hajaufuta wimbo huo.

Wimbo ambao mpaka sasa una shika namba moja Trending YouTube, Wimbo ambao umeangaliwa na viewers milioni 1+.
BASATA kupitia mtandao wao wa kijamii waliandika hivi "Wimbo wa Msanii Ray Vanny wa #Mwanza aliomshirikisha msanii Diamond umefungiwa rasmi kwa kubeba maudhui machafu. Lebo ya Wasafi, wasanii wake sambamba na vyombo vya habari vinapewa onyo na tahadhari kuendelea kutumia wimbo huu kwa namna yoyote ile."


Mpya zaidi Nzee zaidi