F Familia ya Dereva wa John Heche Yaomba Ahadi za Msaada Zitekelezwe Baada ya Kifo Chake | Muungwana BLOG

Familia ya Dereva wa John Heche Yaomba Ahadi za Msaada Zitekelezwe Baada ya Kifo Chake

 


Na Timothy Itembe Tarime.


Familia ya aliyekuwa dereva wa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, imewaomba ndugu, marafiki na wote waliotoa ahadi za kusaidia wakati wa msiba kuhakikisha wanazitekeleza ili kuwasaidia waliobaki na mzigo wa maisha.


Akizungumza wakati wa maombolezo, binti mkubwa wa marehemu, Ackisa Swezi, alisema familia ya Heche ilimchukua baba yake akiwa bado kijana na aliendelea kuitumikia familia hiyo kwa uaminifu hadi alipofariki dunia.


Kwa upande wake, mjane wa marehemu, Swezi Dandel Maradufu, alisema kifo cha mumewe kimemwacha katika kipindi kigumu, akilea watoto wawili pamoja na wajukuu wawili. Alieleza kuwa marehemu alikuwa tegemeo kuu la familia, hivyo pengo aliloacha ni kubwa.


Naye dada wa marehemu, Vashiti, alisema ndugu yake alikuwa mtoto wa tisa kuzaliwa katika familia ya marehemu Dandel Maradufu. Alibainisha kuwa kifo hicho kimewaachia maumivu makubwa, akimwelezea marehemu kuwa alikuwa mtu mwenye upendo, mnyenyekevu na aliyekuwa akijali familia na jamii inayomzunguka.


Alisema familia inaendelea kujiuliza nani atakayeziba pengo aliloacha, kutokana na mchango mkubwa aliokuwa akitoa kwa ndugu na jamaa zake.


Naye diwani mstaafu kata ya Kitembe wilaya Rorya,Thomas Patrick Rissa alisema marehemu alikuwa jirani yake wa eneo analofanyika kazi na amemfahamu kiptia ushirika wa kanisa analo sali la Wasabatho na kuwa wakanisa hao wamehisika katika msiba na alikuwa mtu mpole asiyekuwa na majungu.

Chapisha Maoni

0 Maoni