Utaratibu wa usambazaji pamba wavunjwa na DC Kiswaga


Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga amevunja utaratibu wa usambazaji wa mbegu za pamba unaofanywa na Bodi ya Pamba Wilayani humo, na kuzitaka  kampuni zinazosambaza mbegu hizo kuanza kuwauzia wakulima ili kuondoa tatizo hilo.

Kiswaga amefikia uamuzi huo  wa kuvunja utaratibu huo Leo, wilayani kwake baada ya kuona bodi ya pamba imeshindwa kusimamia zoezi hilo na kuwasababishia wakulima kukosa mbegu .

Aidha Kiswaga amesema kamwe hawezi kuona wakulima wake wanakosa mbegu hizo  kwani uongozi wa Mkoa na Wilaya ulifanya  jitihada kubwa za kuwahamasisha wakulima kulima zao hilo hivyo atarajii kuona wakulima wanakosa mbegu.

Pia ameiagiza Bodi ya pamba kuzisaidia kampuni za usambazaji pamba zilizopo Wilayani Bariadi kwa kuzipa vibali ya uuzaji mbegu kwa wakulima ili zoezi  hilo lianze mara moja

Ameongeza kuwa hadi kufikia mwanzoni mwa wiki ijayo,kampuni hizo ziwe tayari zimeshaanza kuwauzia wakulima mbegu ili waweze kutimiza mahitaji yao.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items