Magonjwa yanayoweza kumpata mwanaume mwenye upungufu wa nguvu za kiume

Zipo sababu mbalimbali ambazo huchangia wanaume kukosa nguvu za kiume, miongoni mwa sababu zinazochangia kukosekana kwa nguvu za kiume ni pamoja unwaji wa pombe kupindukia, mfadhikjo (stress), ualiji wa vyakula pasipo kufuata ushari wa talaamu wa lishe na tiba, unene kupita kiasi na sababu zinginezo.

Pamoja na kuwapo na tatizo hili,  ambalo limekuwa likizungumzwa na watu wengi, watu hao wamekuwa wakitafuta suluhisho kwa waganga wa kienyeji huku wakidhani wapo sahihi kumbe laaa, leo hii kila kibao cha mganga wa kienyeji  kimeandikwa tunatibu nguvu za kiume kitendo hiki kimekuwa kikisababisha watu wengi kutupa fedha zao huku tatizo hilo kubakia palepale.

Hivyo kama unakabiliwa natatizo hili ni vyema ukahakikisha ya kwamba unakwenda kwa watalamu wa afya ili uweze kupata tiba sahihi juu ya tatizo hili.

Lakini pia utafiti uliofanywa hivi karibuni unaonesha kuwa wanaume wenye tatizo la nguvu za kiume pia hukabiliwa na magonjwa mengine.

Inaelezwa kuwa wanaume wenye mbegu chache za kiume wanakabiliwa na tatizo la mafuta mengi mwilini, shinikizo la damu pamoja na mafuta machafu katika mishipa ya damu.

Kutokana na utafiti huu, wanaume wanashauriwa kuhakikisha wanafanya vipimo vya magonjwa mengine ili wawe salama zaidi.