"Wasanii wanaojiunga CCM wakati wa uchaguzi ni wajaza matumbo"

KATIBU MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM), DK. BASHIRU ALLY.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally, ameendelea kusisitiza chama hicho hakitatumia tena wasanii katika kampeni zake, akieleza kuwa wamekuwa wakijiunga nacho wakati wa uchaguzi kwa lengo la kujaza matumbo yao.

Ameyasema hayo leo alipohutubia wananchi katika ziara yake mkoani Geita.

Dk. Bashiru amesema badala ya kutegemea wasanii wanaojiunga na chama wakati wa kampeni tu kwa lengo la kupata fedha, chama kinapaswa kuwa na vikundi vya uhamasishaji na watu wanaojitolea.

Inadaiwa chama hicho kilitumia mabilioni ya shilingi kuwalipa wasanii walioshiriki kampeni zake za uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na 2015.

Katika hatua nyingine, Dk. Bashiru Ally, amesema anayo majina ya wakuu wa mikoa wanne walioanza kampeni za kuchaguliwa kuwa wabunge mwaka 2020.

Amesema kuwa baada ya kumaliza ziara hiyo, atakutana na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli kumkabidhi majina hayo ili wahusika wachukuliwe hatua.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items