Baada ya kutolewa SportPesa Cup, Kocha Yanga SC awapa kazi Simba SC


Kocha Mkuu wa Yanga SC Zahera Mwinyi baada ya timu yake kutupwa nje ya mashindano ya SportPesa, ameitakia kila la kheri Simba SC kufanya vizuri.

Kocha huyo akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa anaumia kuona timu za Tanzania zinatolewa, hivyo kuwataka Simba SC ufanya vizuri kwenye mashindano hayo kama sehemu ya uwakilishi.

"Siwezi kuumia sana kwa jinsi wanatutoa ila naumia kuona jinsi hakuna tena timu ya Tanzania, tunamtakia Simba SC kheri atuwakilishe vizuri," amesema.

Hapo jana Yanga SC walitupwa nje ya mashindano hayo mara baada ya kujikuta wakiambulia kipigo cha goli 3-2..
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items