Baada ya mapicha kibao, Linex na Lady Jaydee wafanya yao


Hatimaye Linex ameachia wimbo wake mpya aliomshirikisha Lady Jaydee. Wimbo huo mpya ambao umetengenezwa na Producer Tony Drizzy unakwenda kwa jina la Too Late.

Huu ni wimbo wa kwanza kwa Lady Jaydee kusikika kwa mwaka huu tangu alipotoa wimbo 'Boyfriend wa Dar es Salaam ulitoka Novemba 2018.

Ni wimbo wa pili kutoka kwa Linex ndani ya mwaka huu baada ya ule uitwao Sinema ambao amewashirikisha Wyre kutokea nchini Kenya na Belle 9.

Hivi karibuni Linex na Lady Jaydee wamekuwa wakifululiza kuweka picha kwenye mitandao ambazo zinatokana na utengenezaji wa video hiyo ambayo pia wameeleza kuwa ipo mbioni kutoka.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items