DC Muro avalia njuga ujenzi wa madarasa Arumeru


Mkuu Wa wilaya ya Arumeru,  Ndugu Jerry Muro amendelea na ziara yake ya kukagua ujenzi wa madarasa kwaajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza katika kata ya Olosiva Halmashauri ya Arusha Dc.

Dc Muro akiwa katika ziara hiyo ameeleza kuwa wanafunzi zaidi ya 617 mpaka sasa wote waliopangwa kuingia kidato cha kwanza mwaka 2019 katika shule ya Sekondari Kiranyi wamepata nafasi ya  kuendelea na masomo yao bila hata mmoja wao kukosa.

Ziara  ya Mkuu wa wilaya  Ndugu Jerry Muro  ni maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo mara baada ya kufanya ziara katika shule ya Sekondari Kiranyi na kumuagiza Mkuu wa Wilaya ya Arumeru kuhakikisha ndani ya wiki mbili wa namalizia moja ya jengo ili kuhakikisha  Elimu bora inatolewa kwa wanafunzi wote  waliochaguliwa kidato cha kwanza kwa mwaka huu.

Pia Dc Muro amempongeza mdau wa maendeleo Bi. Ester Compasion kwa juhudi zake kwa kushirikiana na marafiki zake wamewezeshwa ujenzi wa darasa hilo kwa wiki mbili.

Sambamba na hapo,  Dc Muro amewataka  wananchi wa kata ya Kiranyi katika Halmashauri ya Arusha Dc kwa jitihada zao ambazo wameonyesha kwa kuanza kuchangishana kwa  kuanza ujenzi wa madarasa Sita


Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia