Na Ahmad Mmow, Lindi
Baadhi walinzi wa shule za msingi za manispaa ya Lindi wameuomba uongozi wa manispaa hiyo uwalipe mishahara yao ya miez kumi. Walinzi hao walitoa malalamiko na ombi hilo jana walipozungumza na Muungwana ofisini kwao.
Mwenyekiti wa walinzi hao, Salumu Abdallah amesema halmashauri ya manispaa Lindi mwaka 2010 iliajiri walinzi 31 wa shule za msingi kwa mikataba ya muda mrefu, hata hivyo tangu muda huo ulipaji wa mishahara hauridhishi.
Alisema jumla ya Tsh. Million 17 zinazotokana na mishahara ya miezi kumi hazijalipwa hadi sasa hali inayosababisha waendelee kuisha katika hali ngumu kiuchumi.
Akijibu malalamiko na ombi la walinzi hao kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Ofisa Elimu wa shule za msingi manispaa ya Lindi, Huseni kitingi alikiri kuwepo kwa deni la walinzi hao, Hali inayotokana na kuwepo sheria ya elimu bure inayozuia wazazi na walezi kuchangia elimu.
