Hakuna mtu asiyejua mimi ni msanii mkubwa - Linex



Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Linex amesema kuwa hawezi kuwa star mara mbili kwasababu ukishakuwa umekuwa.

Linex ameiambia EATV amesema kuwa hakuna mtu asiyejua yeye ni msanii mkubwa.

"Siwezi kuwa star mara mbili kwasababu ukishakuwa umekuwa , niwe na single mpya nisiwe nayo na deserve kupata kitu chochote kinachohusiana na sanaa hii, nani asiyejua kama Linex anajua kuimba unataka niimbe nini sasa hivi," alisema Linex.

"Labda nitoe single mpya kuapdate mziki wangu, hakuna mtu ambaye hajui mimi ni msanii mkubwa, sauti yangu ina fiti kwenye muziki wowote."
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia