Kocha wa klabu ya Yanga Mwinyi Zahera amesema uchovu wa Ligi Kuu Bara umechangia timu hiyo kuyaaga mashindano ya SportPesa Super Cup baada ya kuchapwa kwa mabao 3-2 na klabu ya Kariobangi Sharks kutoka Kenya.
“Mechi zipo karibu sana, tumetoka Shinyanga na kufikia mazoezi halafu mechi. Ukingalia hawa hata hawakufanya jambo kwa karibu siku nne,” alisema Zahera raia wa DR Congo.
“Lakini hiyo bado siwezi kufanya kama kisingizio, najua hapa watasema najitetea lakini ni uhalisia. Tumetoka na tuwapongeze walioshinda.”
Kariobang kutoka Kenya waliongoza hadi mabao 2-0 wakati wa mapumziko. Yanga walipata bao kupitia Amissi Tambwe lakini Wakenya hao wakaongeza bao la tatu.
Yanga walifunga bao dakika za mwisho kabisa na kufanya iwe 3-2, juhudi za kusawazisha zikapamba moto, hata hivyo haikuwezekana.