Jaji Mkuu afunguka Kesi ya Zitto Kabwe kukataliwa



Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma, amemsifu Msajili aliyesimama kidete kukataa kusajili kesi ya Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe iliyokuwa inadaiwa kuwa na dosari.

Prof. Ibrahim ametoa sifa hizo wakati akizungumzia wa habari kuhusu wiki ya Sheria.

"Namsifu Msajili aliyesimama kidete kukataa kusajili kesi yenye dosari, nampongeza kwa ujasiri. Kuna makosa ya kibinaadamu, lazima marekebisho yafanyike. Kesi ile ya juzi haikuwa ya kwanza wala ya pili," amesema.

Kesi ya Zitto Kabwe ilikuwa ni ya kupinga kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, CAG, Prof. Mussa Assad kuitwa na kuhojiwa kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia