Kocha wa Cardiff City ataka kujiuzulu kisa kupotea kwa mchezaji wake


Baada ya kutokea tukio la kupotea kwa ndege ndogo binafsi iliyokuwa imembeba mchezaji mpya wa Cardiff City Emiliano Sala, Kocha mkuu wa Cardiff City Neil Warnock ametangaza jambo la kushangaza kidogo kufuatia tukio hilo.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 70 ambaye amedumu katika kazi ya ukocha kwa takribani miaka 40 amesema anafikiria kustaafu kazi ya ukocha kutokana na tukio hilo lililotokea na kusema kuwa amekuwa na wiki ngumu sana.

“Nimekuwa katika kazi ya uongozi wa soka kwa miaka 40 sasa, ninafikiri hiki ndio kipindi changu kigumu sikuwahi kupitia katika kazi hii, nikimuangalia Romina (Dada wa Sala) na familia yao najua wapo katika wakati mgumu, ninawafikiria watoto wangu ningefanyaje sasa kama ingenitokea mimi vile vile, kuhusu kustaafu kwa hili nilifikiria karibia saa 24 kwa siku wiki iliyopita hata hapa nilipo hilo nalifikiria” alisema kocha Neil Warnock


Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items