Na.Ahmad Mmow, Lindi.
Hali mbaya ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea imesababisha Madiwani wa Halmashauri hiyo kuomba walipwe posho zao kupitia fedha za marejesho za mfuko wa vijana na wanawake.
Hayo yalijiri jana wakati wa mkutano wa kawaida wa robo ya pili ya mwaka wa fedha wa 2018/2019 wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, kilichofanyika kwenye ukumbi wa ofisi za Halmashairi hiyo zilizopo katika mamlaka ya mji mdogo wa Nachingwea.
Mtu wa kwanza kuibua hoja hiyo alikuwa ni Diwani wa kata ya Nditi,Abdallah Mkane(CCM) ambae alisema madiwani hawajalipwa posho zao kwa muda mrefu.Hali inayosababisha wawe na maisha magumu na kusababisha kuhudhuria vikao kwa kutumia fedha zinazotokana na vyanzo vingine ambavyo kwa hali ilivyo sasa vimejifunga.
Mkane alisema kutokana na hali hiyo kunahaja ya kutafutwa njia itayoweza kuwafanya walipwe posho zao haraka ili waondokane na hali ya sasa,ambayo aliita kuwa ni mbaya.
Maelezo ya Mkane yaliungwa mkono na diwani wa viti maalumu wa kata ya Mpiruka,Veronica Makota(CCM) ambaye alisema wanatambua hali hiyo inasababishwa na halmashauri hiyo kutokuwa na fedha zinazotokana na vyanzo vyake vya ndani.Hata hivyo zipo fedha za maresho ya mfuko wa vijana na wanawake.Hivyo aliomba fedha hizo zitumike kuwalipa.
Makota alitilia nguvu ombi hilo kwakusema wataalamu wa halmashauri hiyo waliwahi kusema fedha hizo hazina mwongozo,kwahiyo zinaweza kupangiwa matumizi na halmashauri.Hivyo ni vema zitumike kuwalipa posho zao.
"Mnasema fedha hizo nizamaendeleo haziwezi kubadilishwa matumizi.Lakini kuna shilingi 79 milioni zilizorejeshwa zimetumika katika ujenzi wa kituo cha mabasi ambacho ujenzi wake unatokana na fedha za ndani.Kwanini mlipeleka kule ambako ujenzi wake unatokana na fedha za ndani.Sasa kama mliweza kufanya hivyo, kwanini ishindikane kutumika kulipwa sisi,"alihoji Makota.
Licha ya Makota na Madiwani wengine waliotaka fedha hizo zitumike kuwalipa posho,kushangiliwa na takribani na madiwani wote.Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Ahmad Makoroganya alisema nijambo lisilowezekana fedha hizo kutumika kulipana posho.
Alisema hakukuwa na ubaya wowote kwa shilingi 79 milioni zilizorejeshwa kutumika kwa ujenzi wa kituo kipya cha magari ya abiria.Kwani kiasi hicho cha fedha kimetumika kwa shuguli za maendeleo.Hatahivyo haimaanishi kwamba hazikutumika kwa shuguli za maendeleo na wanaweza kutumia kwa matumizi yakawaida.
Alisema sababu inayosababisha madiwani hao kutolipwa ni akaunti ya matumizi ya kawaida kutokuwa na fedha.Hali ambayo inasabishwa na halmashauri hiyo kutopata fedha za ushuru wa korosho.Kwahiyo wavumlie hadi hali ya mapato itakapokuwa njema.
"Hata wajumbe wa kamati ya mipango na fedha hawalipwi wanapofanya vikao vya kila mwezi.Hali yetu kimapato sio njema.Msidhani wanapokutana kila mwezi wanalipwa,"alisisitiza.
Maelezo ya mwenyekiti huyo yaliungwa mkono na baadhi ya watendaji wa halmashauri hiyo akiwemo mkaguzi wa ndani,Kenneth Mwangama ambaye alisisitiza.
