Mke amenipa 'vibe' ya dakika 1 kuhisi kama nimekaa nae miaka 30 - Fid Q


Msanii wa Hip Hop, Fareed Kubanda “Fid Q”, ameeleza sababu zilizofanya kumuoa Mke wake (Mama Cheusi) huku akimmwagia sifa mke wake huyo.

Fid amesema kuwa wana miaka mitatu na mkewe huyo ambaye walianza kama wapendanao ambapo ameeleza kuwa kwenye maisha unaweza kukutana na mtu ndani ya dakika 1 kuhisi kama nimekaa nae miaka 30 ndivyo ilivyo kwake na mkewe.

"Mimi na Mke wangu mama Cheusi tuna miaka kama mitatu hivi tulianza kama wapendanao ni muda mchache kuna vitu vingi tulipitia kiasi kwamba tukajua kama sisi tunajuana kwa takribani miaka 30. Ujue katika maisha kuna kitu cha ajabu sana unajua unaweza kukutana na mtu ndani ya dakika 1 kuhisi kama nimekaa nae miaka 30," alisema Fid Q.

"So Mama Cheusi alinipa hii vibe hii nyingine ya mtu wa dakika 1 kuona umekaa nae kwa miaka 30 kwamba tunajua kwa vitu vingi  tuna Similarities nyingi na different ni chache sana ndio kilichosababisha nikamuelewa haraka," aliongeza Fid kwenye mahojiano yake na Clouds Tv.



Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia