Mkutano wa Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanyika Februari Mosi


Mkutano Maalum wa 38 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unafanyika Arusha kwa lengo lakujadili na kukubabaliana na agenda mbalimbali zitakazowasilishwa kwenye
Mkutano wa 20 wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hiyo utakaofanyika Februari Mosi mwaka huu.

Mkutano huo utajadili agenda mbalimbali muhimu ambazo ni pamoja na ripoti ya utekelezaji wa maamuzi mbalimbali yaliyofikiwa na Baraza hilo kwenye vikao vilivyopita; taarifa kutoka Ofisi ya
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, taarifa kuhusu masuala ya miundombinu, forodha na biashara na ripoti ya kamati ya utawala na fedha.
Agenda zingine ni taarifa ya Baraza kwa Wakuu wa Nchi kuhusu utekelezaji wa maamuzi
mbalimbali yanayofiwa kwenye mikutano ya Wakuu hao wa Nchi na Kalenda ya
Matukio ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Juni 2019.

Ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo  unaongozwa na Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kuwahusisha pia Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (Mb), Waziri wa , Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), Waziri Fedha na Mipango, Mhe. Kapt. Mstaafu George Mkuchika (Mb), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mhe. Joseph Kakunda (Mb), Waziri wa Viwanda na Biashara na Mhe. Innocent Bashungwa, Naibu Waziri wa Kilimo.


Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items