Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amemfukuza kazi askari wa jeshi la polisi aliyekuwa akihudumu kwenye kituo cha Malinyi, PC Hamisi mwenye namba G.7381.
PC Hamisi ametimuliwa kazi kwa kuhusika kwenye udanganyifu wa mitihani ya kidato cha nne iliyofanyika mwaka jana. Askari huyo alikuwa mmoja wa maafisa usalama waliokuwa na jukumu la kusimamia mitihani hiyo.
