Msanii wa Bongo Fleva, Bill Nass amesema bunduki anayoonekana ameishika, Mai (mtoto wa Anko Zumo) kwenye video ya wimbo wake mpya, Funga Geti ni ya bandia.
Bill Nass akizungumza na Clouds FM amesema licha ya bunduki hiyo kuwa feki pia hakumruhusu mtoto huyo kuishika ndio maana alimnyang'anya.
"Na ukitaka kujua kuwa ni toy ndio maana Mai aliishika kwa mkono mmoja, bunduki halisi ina
kilo nyingi asingeweza kuibeba,’ amesema Bill Nass.
Wimbo Funga Geti Bill Nass amemshirikisha Roma ukiwa ni wimbo wake wa pili kufanya na msanii mwingine wa hip hop baada ya Mazoea aliofanya na Mwana FA.
