Msanii kutokea WCB, Rayvanny ameeleza kuwa kufungia kwa wimbo wake 'Mwanza' amechukulia ni kama sehemu ya kujifunza na sio maumivu.
Akizungumza na Wasafi TV Rayvanny ameeleza kuwa hajutii chochote bali anajua kila kitu hutokea kwa sababu.
"Nilijisikia vibaya lakini ujue kila kitu kinatokea kwa sababu aidha ya kujifunza au kukumbushana jambo, kwa hiyo kwangu mimi sichukulii kama sehemu ya maumivu naichukulia kama sehemu ya kujifunza," amesema Rayvanny.
Wimbo 'Mwanza' ambao Rayvanny amemshirikisha Diamond Platnumz ulifungiwa na Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kutokana na kukiuka maadili.
