TANZIA: Mvumbuzi wa Madini ya Tanzanite afariki dunia


Mzee Jumanne Ngoma ambaye aligundua Madini ya Tanzanite amefariki leo  January 30, 2019  katika Hospital ya Muhimbili alipokuwa anapatiwa  matibabu.

Mtoto wa marehemu, Hassan Ngoma amesema, “Ni kweli Mzee amefariki leo jioni hii hapa Muhimbili,” amesema Ngoma.

Mwaka jana, Rais John Magufuli akizindua ukuta wa mgodi wa Tanzanite, Mirerani mkoani Manyara alimzawadia Sh.100 milioni kama shukrani kwa mchango wake kwa kugundua madini hayo.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia