Zaidi ya Sh.milioni 60 kutoka Mfuko wa Jimbo la Babati vijijini, wilayani Babati, Mkoani Manyara zimegawiwa kwenye kata 25 za jimbo hilo ili kuweza kuchangia kasi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Jimbo la Babati vijijini linaongozwa na Mbunge wa CCM, Jitu Son.
Kwa mujibu wa Mbunge huyo ameiambia Muungwana Tv kuwa fedha hizo ambazo zinatolewa na serikali ya chama cha Mapinduzi kwa ajili ya mfuko wa jimbo zimetumika kununua Mifuko ya Saruji ambayo imeelekezwa kwenye kata 25 za jimbo la Babati vijijini ambayo itatekeleza miradi ya ujenzi na ukarabati wa madarasa ya shule ya msingi na Sekondari pamoja na zahanati.
TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI....USISAHAU KUSUSBSCRIBE
