Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amepokea Taarifa ya
kamati maalumu iliyohusisha watu kutoka kada mbalimbali aliyoiunda kwa ajili ya
kuchunguza mauaji ya wanyama pori hasa
Twiga wilayani Longido mkoani Arusha katika kipindi cha miaka miwili.
Akizungumza na wanahabri ofisini kwake Leo Gambo amesema
baada ya kamati hiyo kufanya uchunguzi wa kina ilibaini kuwa katika kipindi cha miaka
miwili 2017/2018; jumla ya Twiga 35
walikufa kutokana na sababu mbalimbali lakini Twiga ambao walikufa kutokana na
sababu za ujangili ni 25
Gambo amesema Kamati hiyo imegundua kwamba moja ya
sababu ambazo zinachangia ujangili wa Twiga kuongezeka kuwa ni pamoja na sababu
za kibiashara; ambapo kamati hiyo ilipata taarifa ya watu wasiopungua 25 ambao
wanatajwa kuhusika na masuala ya ujangili Wilayani Longido.
Aidha Gambo ameiomba wizara ya maliasili na Utalii kuunda
Timu ya uchunguzi kuhusu malalamiko dhidi ya Kampuni ya Uwindaji ya Green
Milles kuhusiana na kitalu kudaiwa na vijiji vinavyopakana kutotengeneza
miundombinu ya barabara na kutofanya doria kwenye kitalu chake..
Kaimu kamanda Mkoa wa Arusha kamishna msaidiz Longinus Tibishubwamu Amesema mpaka
sasa Jeshi hilo linawashikilia Watu 5 huku wakiendelea kuwafatilia wengine 20
ambao wametorokea Nchi jirani ya Kenya nakusisitza kuwa Watu hao Wanawatia
Nguvuni
TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.........USISAHAU KUSUBSCRIBE...........
