Na Rahel Nyabali,Tabora
Wafanyabiashara wa soko la Kachoma liliopo Manispaa ya Tabora mjini mkoani Tabora, wamelalamikia uongozi wa halmashauli hiyo kwa miundombinu mibovu katika soko hilo na kusababisha mazingira ya biashara kuwa magumu.
Wameyasema hayo walipozungumza na Muungwana Blog, katika soko hilo ambalo mazingira yake si rafiki kwa mfanyabiashara na mteja hasa wakati huu wa masika.
Mmoja wa wafanyabiashara Tatu Hamisi amesema wakati wa masika mvua zinaponyesha wanalazimika kufunga biashara kutokana na ubovu wa mabati yanayo pitisha maji.
"Kweli tunateseka sana kuma mimi meza yangu ya biashara iko kalibu na dimbi la maji machafu yanatoa harufumbaya tunaomba uongozi wa halimashauli utuone huluma," amesema Tatu.
Soko la Kachoma nimoja ya solo linalo ingizia kipato Halimashauli ya Wilaya ya Tabora lakini bado lakini bado miundombinu nimibovu na toka enzi za ukoloni halijapata umeme mpaka sasa.
Aidha Katibu wa Soko hilo Ali Kafimbi amesema licha ya viingozi wa halmashauri hiyo kutoa ahadi ya kukarabati soko hilo lakini bado hakuna utekelezaji wowote unaoendelea sokoni hapo.
"hili soko unavyoliona toka lifanyiwe ukarabati mwaka 2011 hadi leo hatujawahi kufanyiwa matengenezo tena licha ya kutoa kodi lakini hatuoni mabadiliko yeyote maji yametuama hali inayo sababisha harufu mbaya," amesema Kafimbi.