Msanii wa Bongo Fleva na Mchezaji wa Coastal Union ya jijini Tanga, Alikiba ni miongoni mwa wa
wachezaji wanaotarajiwa kuwepo kwenye kikosi cha timu hiyo ambacho kitashuka dimbani hapo kesho kuivaa Yanga SC.
Akizungumza na Azam TV amesema kuwa timu yao imefanya maandalizi ya kutosha kutokana Yanga ni timu kubwa kwao.
“Tunazingatia yale mafunzo ambayo tumepewa na mwalimu na kujikita kwenye mchezo, tukicheza kwa umoja (team work) tunaweza kufanikiwa kwa sababu Yanga ni timu kubwa ina uzoefu, hivyo lazima tucheze kwa uangalifu “ amesema Alikiba.
Hapo kesho Coastal Union wanashuka dimbani kuikabili Yanga SC wakiwa nafasi ya tisa katika msimamo wa Ligi Kuu kwa kujikusanjia pointi 28, huku Yanga wakiongoza ligi hiyo kwa pointi 53.
