Vifo vya mama na mtoto vyafikia 54 kwa mwaka mkoani Tanga


Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela ameishauri serikali kuchukuwa hatua za haraka ilikuweza kudhibiti tatizo la vifo vya wajawazito nchini kuepuka kupoteza nguvu kazi kubwa.

Ameyasema hayo wakati Uzinduzi w akampeni ya uwajibikaji katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi mkoa wa Tanga ijulikanayo kama Jiongeze Tuwavushe Salama.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa mkoa huo, Dkt. Asha Mahita aliweza kutaja takwimu za vifo kwa kipindi cha miaka minne ambapo kwa mwaka 2015 jumla ya vifo vilikuwa 67.

“Kwa mwaka 2016 kuliuwa na vifo 46 ,huku mwaka 2017 kukiripotiwa vifo 45,ambapo mwaka 2018 kukiwa na vifo 54,” alibainisha Mganga Mkuu huyo.

Aliendelea kusema, 'Tumejipanga katika kuhakikisha kila wilaya, huduma ya mama na mtoto inakuwa ni kipaumbele chetu lakini pia kutenga bajeti kubwa ili kuweza kutatua kwa haraka changamoto za wajawazito na watoto wachanga,'.

Mpya zaidi Nzee zaidi