BREAKING: Mtoto mwingine auawa Njombe


Mtoto wa miaka 10 ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili ameuawa kikatili na kutelekezwa kichakani Lupembe mkoani  Njombe wakati akitoka shuleni jana.

Tukio hilo linatokea siku kadhaa baada ya Watoto sita, wakiwemo watatu wa familia moja wenye umri chini ya miaka 10 kupatikana wakiwa wamefariki katika mazingira ya kutatanisha mkoani humo.

Siku mbili zilizopita Bungeni, Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Kangi Lugola amesema tayari wameshabaini baadhi ya wale waliohusika na mauaji hayo na hatua kali zitachukuliwa.

Mpya zaidi Nzee zaidi