Na John Walter-BABATI
Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Babati mkoani Manyara Mohamed Kibiki amevuliwa cheo hicho baada ya madiwani kupiga kura za kutokuwa na imani naye.
Wadhfa wa kiongozi huyo umevuliwa Jumanne februari 12.2019 katika kikao maalum kilichoketi ambapo pia mkurugenzi mtendaji wa mji alihudhuria.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya mji huo Fortunatus Fwema ameeleza tuhuma zinazomkabili ni pamoja na utoaji wa zabuni,usimamizi wa fedha za miradi ya maendeleo na asilimia kumi ya mfuko wa vijana,wanawake na walemavu na kushindwa kusimamia vyema vyanzo vya mapato vya Halmashauri ya mji.
Mkurugenzi amesema taratibu zote zimefuatwa kwanza aliandikiwa barua na madiwani,pia yeye akamwandikia barua ya kumtuhumu ili aweze kujibu hoja za madiwani hao ambapo Mwenyekiti huyo alizijibu hoja zote na kupelekwa kwa mkuu wa mkoa na kishja kuundwa tume ya kuchunguza tuhuma na hoja alizozitoa Kibiki.
Baada ya hapo tume iliyoundwa na Mnyeti ilirudisha majibu ambayo yalionyesha tuhuma zote zina ukweli na mkurugenzi kuhitisha kikao hicho na kutolewa maamuzi hayo.
Kumbuka Halmashauri inaongozwa na Chama cha mapinduzi kwa idadi kubwa ya madiwani katika kata sita za Singe,Bagara,Sigino,Bonga,Maisaka na Mutuka ukilinganisha na Chama cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA] yenye kata tatu pekee za Nangara na Babati mjini alipo Mohamedi kibiki aliyevuliwa cheo hicho.
