Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) limeeleza kupokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha Msanii wa Hip hop Bongo, Golden Jacob Mbunda a.k.a Godzilla.
"Wakati tukijipanga kushiriki taratibu zingine na kutoa rasmi salamu za rambirambi kwa wanafamilia, tunatoa pole za dhati kwa familia yake, wasanii na wadau wa sanaa kwa ujumla," taarifa ya BASATA imeeleza.

