Mbunge wa Iramba Magharibi Dk.Mwigulu Nchemba amepata ajali ya gari akiwa njiani barabara ya Iringa kuelekea Dodoma na kukimbizwa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma.
Mkurugenzi wa hospitali ya Benjamin Mkapa Dk.Alphonce Chandika amethibitisha kumpokea Mwigulu na kusema kuwa tayari ameshaanza kupatiwa matibabu ya awali na kufanyiwa vipimo.
Kwa mujibu wa Dk. Chandika amesema mgonjwa alikuwa analalamika maumivu kwenye kifua na kwenye kiuno hivyo wamechukua vipimo ili kujua kama kuna tatizo au la ,lakini mgonjwa anajitambua na anazungumza.

