Kiongozi huyo alipta ajali hiyo akiwa njiani barabara ya Iringa kuelekea Dodoma na amekimbizwa hospitali ya Dodoma. Akiwa Hospitalini hapo ameeleza chanzo cha ajali hiyo.
“Nilikuwa naelekea Singida kwenye kikao cha kamati ya siasa na Wabunge wa mkoa nikiwa natokea Iringa, nilikuwa naongea na simu ghafla wakakatiza punda watatu na sikuwa nimeona," amesema.
Ameendelea kwa kusema, 'Nilishituka tu mara baada ya dereva kutoa ishara ya kwamba kuna kitendo cha hatari,'.

