Dkt. Ndumbaro aagiza kusimamishwa kazi Mkuu wa Idara ya Utumishi


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi,  Dkt.Laurean Ndumbaro amemwagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam kumsimamisha kazi na kumchukulia hatua za kisheria Mkuu wa Idara ya Utumishi wa manispaa hiyo Bernatha Mwaikambo.

Ndumbaro amegiza pia kuwachukulia hatua za kinidhamu maofisa wanaohusika na Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Aidha ameyataja baadhi ya malalamiko ya watumishi wa manispaa kutokuwepo kwa taarifa kamili za upandishwaji vyeo pamoja na uwasilishwaji usioridhisha wa malimbikizo ya watumishi.


Mpya zaidi Nzee zaidi