Na Timothy Itembe Mara.
Halmashauri ya Tarime mkoani Mara kwa mwaka wa fedha 2018/2019 imeshuka mapato ya makusanyo ya fedha kutokana na baadhi ya vyanzo vyake vya mapato kuhamishiwa kwenda Serikali kuu.
Afisa Mipango wa halmashauri hiyo,Magige Samweli aliliambia baraza la madiwani lililoketi jana katika ukumbi wa halmashauri kuwa makusanyo ya mapato kwa mwaka wa fedha 2018/2019 makusanyo yake yalishuka na kuwakuvuka lengo kutokana na baadhi ya vyanzo vyao vya makusanyo walivyokuwa navyo kuhamishiwa kwenda Serikali kuu.
“Katika mwaka wa fedha 2018/2019 halmashauri ya wilaya Tarime iliidhinishiwa kukusanya na kutumia jumla ya Shilingi 37,430,504,436.00 kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato hadi kufikia Desemba 312018 jumla ya shilingi 14231228150.00 zilikuwa zimekusanywa sawa na asilimia 39 ya makusanyo yote”alisema Samweli.
Samweli aliongeza kuwa baadhi ya vyanzo vilivyohamishwa na kusababisha halmashauri hiyo kukusanya mapato na kushindwa kuvuka lengo nipamoja na chanzo cha,Ruzuku ya miradi ya maendeleo (LGCDC) cha makusanyo kuondolewa huku akitaja kingine kuwa ni kuondolewa sekta ya Maji kuwa chini ya Wakala wa Maji.
Kipindi cha mwaka wa fedha 2019/20209 halmashauri inaomba kukusanya na kutumia jumla ya shilingi 31285415688 ya vyanzo mbalimbali vya mapato aliongeza kusema Samweli.
Kufuatia taarifa hiyo mwenyekitio wa halmashauri ya wilaya Yomami Misiwa aliwataka madiwani kujadili na kupitisha Rasimu ya bajeti ya mwaka 2019/2020 kwa umakini.
