Ishu ya Nape kutolea bastola, Dkt. Mwigulu afunguka


Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amefunguka kuhusu tukio la Nape Nnauye kutolewa bastola na mtu anayedaiwa kuwa askari.

Ni kipindi ambacho Dkt. Mwigulu akiwa Waziri na siku ambayo Nape aliondolewa kwenye wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo alipokuwa waziri wa wizara hiyo.

Kwenye mahojiano na kipindi cha Clouds 360 kinachoruka Clouds TV, Dkt. Mwingulu amesema jambo lolote lina taratibu zake za kushughulikiwa sio kila kitu huwa kinatangazwa.

"Sikuwahi kusema sio askari, nilisema sio polisi, nilimwelekeza IGP kuchukua hatua aliniambia yule jamaa sio polisi, kuna utaratibu wa kuchukua hatua sio kila hatua inatangazwa kwenye vyombo vya habari,"

Utakumbuka July 2018 Rais John Magufuli alifanya mabadiliko madogo katika baraza lake la Mawaziri, ambapo ameteua Kangi Lugola (aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira), kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Mwigulu Nchemba.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items