Uongozi wa Simba SC wajipanga kuimaliza Al Ahly kesho


Uongozi wa Simba SC umefunguka kuwa wamejipanga vizuri ili kuhakikisha wanatimiza ahadi yao ya kubakiza pointi tisa za nyumbani katika michezo ya Ligi ya Mabingwa ambayo itachezwa na JS Saoura na sasa ni zamu ya Al Ahly ya Misri.

Timu ya Simba inatarajiwa kucheza na mwarabu wa Misri Al Ahly Kesho Uwanja wa Taifa saa 10:00 jioni ambapo kiingilio kwa jukwaa la mzunguko ni shilingi elfu mbili tu.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema wanatambua mashabiki wengi wana maumivu hasa baada ya kushindwa kufanya vizuri katika michezo yao miwili ya ugenini sasa ni muda wao wa kulipa kisasi.

"Tunajua namna gani ambavyo mashabiki wanaumia kutokana na matokeo mabaya ambayo tuliyapata Misri, ila tuna nafasi ya kufanya vizuri na kupata matokeo kikubwa ni wana Simba kuungana na kuishangilia timu yetu. amesema Manara

Hata hivyo amesema Mwaka 1985 walikuta na mabingwa hao katika Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza na waliwafunga mabao 2-1 tena wakati huo ilikuwa ni moto wa kuotea mbali zaidi ya sasa  kama iliwezekana wakati ule kwa nini jumanne isiwezekane.