Kocha wa Alliance FC aipiga mkwara Azam FC

Kocha wa timu ya Alliance FC, Malale Hamsini amesema anatambua ushindani uliopo Ligi Kuu Bara na baada ya kuwashushia kichapo cha mabao 2-0 Lipuli ya Matola akili zake ni kwa Azam ya Hans Pluijm.

Hamsini amesema anatambua ubora wa kikosi cha Azam FC pamoja na ubora wa mwalimu wao ila hilo halimpi kazi.

"Tunajua kazi yetu ni kutafuta matokeo kwenye michezo yetu yote inayofuata hivyo haijalishi tutakutana na timu ya aina gani hesabu zetu ni ushindi.

"Najua tutakuwa ugenini lakni kwenye mchezo wa mpira haijalishi unaanzia wapi iwe nyumbani ama ugenini kikubwa ni mipango tu, nawajua Azam FC kikosi changu kitafanya maajabu kwenye Uwanja wa Chamazi," alisema Hamsini.

Alliance wanashika nafasi ya saba wakiwa na pointi 31 kwa sasa wamekuwa na mwenendo mzuri kwenye kwa kupata matokeo ambayo yanaweka kwenye kumi bora katika msimamo.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items