Kocha wa Yanga SC, aamua hatima ya Amis Tambwe


Kocha Mkuu wa Yanga SC, Zahera Mwinyi amelazimika kumpumzisha mshabuliaji wa kikosi hicho, Amisi Tambwe mazoezi ya leo asubuhi ili apate wasaa wa kurejea vyema kiafya.

Hii ni baada ya  kupasuka na kushonwa nyuzi 5 baada ya kugongana na kipa wa Biasharamara FC, Nurdine Abarora kwenye mchezo wa Azam Sports Federation Cup (ASFC) uliochezwa Jana uwanja wa Taifa.

Hata hivyo kocha Zahera Mwinyi amethibitisha kuwa mshambuliaji huyo atakuwa sehemu ya kikosi
kinachosafiri kwenda jijini Tanga na Singida kwa ajili ya michezo mitatu ya ligi inayofuata.

Hadi sasa Yanga SC inaongoza Ligi Kuu Soka Tanzania (TPL) ikiwa na pointi 53 kibindoni na wakiwa wamecheza michezo 20.
Mpya zaidi Nzee zaidi