Mwanaume wa Ethiopia ''aliyefufuka'' wakati wa mazishi yake miezi miwili iliyopita amefariki dunia.
Hirpha Negero alithibitishwa kufa mwezi Novemba ambapo aliwekwa ndani ya jeneza kwa saa tano, lakini wakati wa mazishi yake wanavijiji walisikia akigonga jeneza.
Bw.Hirpha alisimulia BBC yaliyomfika wakati huo na kusema kuwa alimsikia mtu akilia alijihisi kuishiwa na pumzi ndipo akajaribu kujitoa katika hali hiyo na alikuwa mnyonge hata hakuweza kuzungumza baadae alifanikiwa kuwaita watu.
Mchimba kaburi Etana Kena alisema watu walishtushwa na tukio hilo na wote walikimbia na kuliacha jeneza ilibidi ajifungulie mwenyewe baada ya kisa hicho hafla ya mazishi iligeuka kuwa sherehe.
Mchimba kaburi wa awali alimzika tena Hirpha kwa mara ya pili siku ya Alhamisi, siku moja baada ya kifo chake.
