Waarabu wamuundia tume Okwi



Wakati mechi ya kimataifa ya mabingwa Afrika kati ya Simba na Al Ahly ikizidi kupamba moto, imebainika kuwa mshambuliaji wa Simba SC Emmanuel Okwi ndiye mchezaji anayewapasua vichwa vilivyo viongozi wa benchi la ufundi la Waarabu hao.

Hiyo ni kutokana na rekodi nzuri aliyonayo dhidi ya timu za Waarabu ambapo kila ana­pokutana nao uwanjani mara nyingi amekuwa akiwasumbua.

Kiungo mshambuliaji wa Simba, Haruna Niyonzima amesema kuwa mara tu baada ya kufika Misri walipata taarifa kuwa Okwi ndiye anaye­waogope­sha zaidi Waarabu hao na tayari beki wa zamani wa TP Maz­embe ya DR Congo, Mmali, Salif Coulibaly ambaye anawatumikia Waara­bu hao kwa sasa, amepatiwa jukumu la kumdhibiti.

“Hiyo ndiyo taarifa mpya ambayo tumeipata hivi kar­ibuni, lakini tunaendelea vizuri na maandalizi yetu na katika mechi hiyo ya Jumamosi tuta­pambana vilivyo kuhakikisha tunafanya vizuri.

Hata hivyo Niyonzima amesema wao wanaitaji ushindi katika mchezo huo na kama siyo ushindi basi sare lakini siyo kupoteza mch­ezo huo, pamoja na kumuwekea ulinzi mkali Okwi bado wanaamini watafanya vizuri.

Mpya zaidi Nzee zaidi