Msanii wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda amesema ni kweli alishuka kimuziki kutokana na matatizo
kwenye mahusiano yake ya kimapenzi.
Muimbaji huyo akizungumza na Clouds FM amesema kitendo cha kuachana na mkewe, Nawal kilishusha sana uwezo wake wa kufanya kazi kwa kiasi kikubwa.
"Mapenzi ndiyo sababu kubwa ambayo iliniua kimuziki maana wakati nipo kwenye ndoa kuna mambo mengi yalitokea mpaka kufikia hatua ya kuachana na ile mivutano ya hapa na pale baina yangu na aliyekuwa mke wangu," amesema Nuh.
"Yalinipa msongo wa mawazo sana na kukuta napoteza nguvu za kufanya muziki kama zamani na
hiyo ndiyo sababu hata iliyopelekea mimi kuandika wimbo wa Natapatapa kwani," ameeleza.
Kabla ya Nuh kuingia kwenye ndoa alikuwa akitoka kimapenzi na msanii mwenzake, Shilole ambapo walifikia hata hatua ya kuunda kundi la muziki ambalo walilipa jina la Shiwanda.
