Picha : Rais Magufuli aipa Channel Ten Milioni 200


Mwenyekiti wa Chama cha Mapiunduzi (CCM) na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, ametimiza ahadi yake ya kutoa shilingi milioni mia mbili  kama alivyoahidi jana kwa wafanyakazi na watumishi wa kampuni inayomilikiwa na chama cha mapinduzi  ya afrika media group limited yenye vituo vya habari vya runinga na radio ikiwemo channel Ten,Dtv na Ctn pamoja na radio ya Magic Fm.

Katibu wa NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga akimsikiliza mmoja wa wafanyakazi wa Channel Ten Bi. Siri Pambe akisoma hundi ya Shilingi Milioni 200 kabla hajaikabidhi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya African Media Group Limited (AMBL) Jaffari Haniu kama ilivyoahidiwa jana na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ili kununua vifaa kuimarisha utendaji wa televisheni hivyo. Akishuhudia kulia ni Katibu wa Mwenyekiti wa CCM Ndg. Ngusa Samike
Katibu wa NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya African Media Group Limited (AMBL) Jaffari Haniu akitoa shukurani baada ya kukabidhiwa hundi ya shilingi Milioni 200 aliyoahidiwa jana na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ili kununua vifaa kuimarisha utendaji wa televisheni hivyo. Akishuhudia kulia ni Katibu wa Mwenyekiti wa CCM Ndg. Ngusa Samike

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia