Wachezaji wa Simba wakifanya mazoezi mepesi kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly utakaopigwa leo.
Simba SC itashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wao mwisho wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi AS Vita ya DR Congo kwa kulala kwa goli 5-0.
Utakumbuka hadi sasa Simba inashika nafasi ya tatu kwenye kundi lao ikiwa na pointi tatu sawa na AS Vita ambayo ina idadi kubwa ya magoli ya kufunga, Al Ahly inaongoza kundi ikiwa na pointi nne.
