Rais Magufuli ampa dawa ya Bundi Spika Ndugai


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai leo amemueleza Rais Magufuli juu ya matukio mawili yaliyotikisa ndani ya Bunge hivi karibuni, ambalo ni tukio la bundi kuonekana na king’ora kusikika hali iliyopelekea kikao cha Bunge kusitishwa kwa muda.

"Jana Bungeni kulilia king’ora cha kuashiria moto, ndani ya muda mfupi ukumbi ulikuwa mtupu, ule upande wa Waziri Mkuu kulikuwa kweupe kumbe tuna wanariadha wengi Bungeni," alisema Spika Ndugai.

Kwa upande wake, Rais Magufuli akitoa hotuba yake amesema kuwa  "Nimemsikia Spika akisema kuhusu Bundi, sijamsikia akizungumzia Fisi zinazozunguka kule Dodoma kama nazo zina matatizo lakini ndio changamoto ya Dodoma. Awapeleke tu viongozi wetu wa dini, Bundi hawezi kuingia kwenye Bunge."

Rais Magufuli ameyasema hayo kwenye maadhimisho ya wiki ya Sheria ambayo yamefanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia