Rais wa Misri achaguliwa kuwa Mwenyekiti wa AU

Rais Paul Kagame na Rais Abdel Fattah al-Sisi 
Rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi achaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa nchi huru za
Afrika (AU).

Hii baada ya Rais wa Rwanda, Paul Kagame kumaliza kipindi cha Ungozi wake kilichodumu kwa
kipindi cha mwaka mmoja.

Hata hivyo Shirika la Amnesty International  limeonya kuwa kuchaguliwa kwa Abdel Fattah al-
Sisi kunaweza kudidimiza haki za binadamu.

Hiyo ni kutokana tangu mwaka 1995 viongozi wa Misri hawakuwa wakiudhuria mikutano ya AU baada ya jaribio la kuuawa kwa aliyekuwa Rais wake wa wakati huo, Hosni Mubarak.

Licha ya hili, wakati akiuhutubia umoja huo nchini Ethiopia, Abdel Fattah al-Sisi amesema kuwa atajikita zaidi katika kuimarisha masuala ya kiusalama.