Na Timothy Itembe Mara.
Mkuu wa mkoa Mara Adamu kigoma Malima ameipa siku tatu halmashauri ya wilaya Tarime kujitathimini juu ya matumizi ya fedha shilingi Bilioni 9.5 wanazopokea kutoka Mgodi wa Nordh Mara kama malipo ya ushuru wa huduma ya miaka mitatu kuanzia mwaka 2015 hadi mwaka 2018
Malima alisema hayo leo mbele ya mkutano ulioitishwa kwa lengo la kumpokea mkuu mpya wa wilaya Tarime,mkutano ambao ulikalia katika ukumbi wa halmashauri na kuhudhuriwa na madiwani wa pande zote mbili na watumishi wa pande zote mbili yaani halmashauri ya Tarime Mji na halmashauri ya wilaya wakiwemo viongozi mbalimbali wa vyana vya siasa,wengine kutoka taasisi za dini huku wakiwemo na wananchi.
Malima aliendelea kusema kuwa halmashauri ya Tarime inapokea pesa kutoka mgodi wa ACACIA kama tozo ya ushuru wa huduma kwa kila miezi mitatu zaidi ya shilingi bilioni moja.
“Ndugu madiwani pamoja na watumishi wote mnahusika katika jambo hilo kwa hali hiyo natoa siku tatu kukaa na kujifungia ndani ili kujitadhimini juu ya matumizi ya fedha mlizopokea kutoka mgodi wa ACACIA kama ushuru wa huduma zaidi ya shilingi Bilioni 9.5 ambapo ndani yake kuna mashaka ya jinsi zilivyotumika fedha hizo”alisema Malima.
Pia Malima aliwataka vyombo vya uchunguzi Takukuruchini ya kamanda wake wa wilaya Daniel Kabakara pamoja na maafisa wa TRA chini ya meneja wake Frank Lwesya kuchunguza fedha hizo na kuleta majibu ya kina ili hatua zingine kuchukuliwa.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya Tarime mpya,Charles Francins Kabeho alisema kuwa alipoteuliwa alikabidhiwa katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania pamoja na Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015 kwa hali hiyo atafanya kazi kwa mjibuwa Katiba na Ilani ya uchaguzi siovinginevyo.
Kabeho aliongeza kuwa katika wilaya Tarime kuna changamoto nyini ikiwemo migogoro ya Ardhi,ukiukwaji wa sheria na haki za binadamu kama vile ukatili,ubakaji,ulawiti,Tohara isiyo salama,rushwa ya ngono kazini na watoto kunyimwa haki Elimu na kuwa yote hayo atakabiliana nayo .
Pia Kabeho alitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais wa jamuhuri ya muungano ya Tanzania wa awamu ya Tano,John Pombe Magufuli kuteua kuwa mkuu wa wilaya Tarime ambapo pia aliomba wananchi kumuunga mkono Rais wa awamu ya Tano katika kupambana na mafisadi,wahujumu uchumi kwa maendeleo ya Nchi ya Tanzania.
Naye mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi mkoa Mara Samweli Keboye maarufu namba tatu alisema kuwa wilaya Tarime ni tajiri lakini katika utajiri wake mkuu wa wilaya huyo anatakiwa kujihadhari na fedha haramu ili kuondokana na baadhi ya watu kumuweka mfukoni.