Mshambuliaji wa Timu ya Yanga SC Amisi Tambwe hatakuwa sehemu ya mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Coastal Union utakaochezwa Februari 3 mwaka huu (jumapili) kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga kutokana na kuwa majeruhi.
Tambwe aliumia jana kwenye mchezo wa Kombe la shirikisho FA dhidi ya Biashara United ambapo katika mchezo huo Yanga iliibuka na ushindi wa penati 5-4 na kufanikiwa kutinga hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.
Mratibu wa Klabu hiyo Hafidhi Salehe amesema kuwa Timu inaendelea vizuri na leo itasafiri kuelekea mkoani Tanga kwa ajili ya mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara, ila Tambwe hatakuwa sehemu ya wachezaji watakao safiri kutokana na majeraha aliyonayo.
.
Tabwe aliumia jana kwenye mchezo wa FA dhidi ya Biashara United, ameshonwa nyuzi 3 kwenye paji la uso lakini sasa anaendelea.
