Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Manyara, Simon Lulu amewapokea na kuwasikiliza wakulima na wafugaji ambao wameungana kwa pamoja kumpongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa hatua yake ya kuwatetea wasisumbuliwe.
Mwenyekiti huyo akizungumza katika viwanja vya CCM kata ya Galapo wilayani Babati, alisema Rais Magufuli amewakuna wafugaji na kuwaonyesha yeye ni mtetezi wa wanyonge.
Akiongea na Muungwana TVmmoja ya watu waliohudhuria kwenye mkutano huo amempongeza Rais Magufuli na kuongeza kuwa ifikapo mwaka 2020 wakulima wote na wafugaji wa eneo hilo wanahamia CCM kutokana na uongozi bora wa serikali ya awamu ya tano.
TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI....USISAHAU KUSUBSCRIBE
